Change Language: English

Utamaduni wa Zama za Kimada:

Na kinachosikitisha ni kwamba binadamu leo hii wanaishi katika kivuli cha utamaduni unaozalisha ubabe na kulea ukatili, utamaduni huu wa kimaada ambao unatilia mkazo ubinafsi na kuchochea matamanio ya mwanadamuna raghba zake, na unaandaa mwelekeo huu kupitia matangazo kwa njia mbalimbali ambazo zinaunga mkono mwelekeo huu. Utamaduni huu ambao unatukuza ubabe na mabavu unapanda mwelekeo huu kwa watu na hasa watoto, kupitia filamu za katuni ambazo nyingi kati yake zina utamaduni wa mabavu na mafunzo ya ukatili.

Zaidi ya hapo ni kwamba vitendo vya mabavu, ukatili, umwagaji damu, na mauaji holela havipingwi kama ilivyokuwa katika wakati uliopita. Kila siku katika matangazo ya habari mwanadamu anaona maiti, mauaji na uharibifu, mwonekano huu ambao katika wakati uliopita mwanadamu alikuwa anaanguka kwa kusikia tu achia mbali kuona, leo umekuwa ni jambo lenye kuzoeleka na la kawaida kwa mdogo na mkubwa, mwonekano huu unazalisha ubabe na ukatili na kuutangaza katika jamii. Na kwa sababu hiyo jamii mbalimbali zinakabiliwa na ukatili na makosa ya jinai.

Katika kila sekunde mbili na nusu Marekani kunatokea kosa la jinai. Na yanatokea matukio zaidi ya elfu tano ya makosa ya jinai ndani ya Marekani yaliyopangiliwa. Katika matokeo ya utafiti uliyofanywa katika kundi kubwa la Wamarekani walioulizwa: Ni matatizo yapi makubwa ambayo mnakabiliana nayo? Asilia 21 walijibu: Ni makosa ya jinai ya ukatili na utumiaji nguvu. Na asilimia 40 ya Wamarekani wanalazimika kubadilisha muundo wa maisha yao kwa kuogopa kufanyiwa makosa ya jinai na kwa kuogopa waovu.

Jamiiyetu kwa kuizingatia kuwa ni sehemu ya ulimwengu huu na inaunganishwa kupitia vyombo vya habarina mawasiliano ya kijamii, na sisi tumekuwa tunaishi na matatizo kama hayakatika jamii zetu.

Utumiaji Nguvu na Kutishiwa kwa Amani ya Jamii:

Hali ya mabavu inapokuwa ni ya kawaida kwa watu, na wanapowatukuza wenye ubabe badala ya kusimama pamoja na anayedhulumiwa, hapa amani ya jamii huwa katika hatari. Wakati ambapo utamaduni wa Kiislamu unaamuru jamii kushikamana pamoja na aliyedhulumiwa na kumshutumu dhalimu, Qur'an tukufu inaendelea milele kulaani dhulma iliyotokea kabla ya maelfu ya miaka, kosa la jinai walilotendewa kundi la waumini pasi na haki, anasema (swt):

"Naapa kwa mbingu yenye Buruji! Na kwa siku iliyoahidiwa! Na kwa shahidi na chenye kushuhudiliwa! Wamelaaniwa watu wa mahandaki." (Surat Buruji: 1- 4).

Hivi ndivyo Qur'an inavyoonyesha tukio hili kwa ukubwa huu. Na sisi tunapokumbuka mateso na dhulma iliyotokea kwa Ahlulbayt hakika ni kwa ajili ya kuimarisha nguzo hii, nayo ni: Kushikamana pamoja na waliodhulumiwa.

Na mkabala wa hili kuna utamaduni unaowatukuza madhalimu na wala haupingi wanayoyafanya miongoni mwa dhulma, na anapokufa dhalimu inamtosheleza shahada mbili.

Na katika baadhi ya vitabu vya turathi tunakuta baadhi ya maneno ya kushangaza, katika kitabu cha Tahadhib, kwa mfano kuna riwaya kutoka kwa Umar bin Sa'ad na katika maelezo inasemwa juu yake kwamba: “Umar bin Sa'ad ni taabi'i mkweli, alimuuwa Husein.”Kana kwamba kosa la kumuuwa Imam Husein si chochote wala halipelekei kuporomosha uaminifu wa mwenye kulitenda!!

Amani ya Jamii Yetu Inaelekea Wapi?

Amani ya jamii ni maudhui muhimu sana, mwanadamu anatarajia kuishi katika jamii ambayo humo anapata amani katika nafsi yake, mali yake na heshima yake, na hili ni jambo muhimu katika furaha ya mwanadamu. Katika riwaya kutoka kwa Imam as-Sadiq (as) anasema: “Neema ya duniani ni amani na afya ya mwili. Na neema iliyo kamilifu akhera ni kuingia peponi.

Katika wakati uliopita amani katika jamii yetu ilikuwa inapatikana kwa wingi, watu walikuwa na amani katika nafsi zao, nyumba zao, familia zao, na mali zao. Ndiyo, haikuwa ni jamii ya malaika hivyo yaliweza kutokea makosa, wizi na uovu, lakini kuna taofauti baina ya kuwa hali hizi ni za mtu mmoja mmoja na ni chache, na baina ya kuwa nyingi na kukaribia kuwa ni hali ya kawaida. Mwanadamu anashangaa kwa anayoyasikia baina ya wakati mmoja na mwingine miongoni mwa uovu dhidi ya nafsi, heshima na mali, hadi inakaribia tusisadiki kwamba haya yanayotokea katika jamii yetu ambayo tulikuwa tunajifakharisha nayo na tunajivunia mbele ya umma zingine. Matukio katika nyanja hii ni mengi na miongoni mwayo ni: Kuwafanyia mabaya wanawake kwa kuibiwa mikoba yao, kuwaudhi wakati wakitembea barabarani na sokoni, na vile vile kuwafanyia mabaya watoto kwa kuwateka, na kuwafanyia mabaya wafanyakazi wa kike wanaoletwa ambao hapo nyuma walikuwa wanahisi utulivu kwa kuwa kwao wafanyakazi katika sehemu hii. Baadhi ya makosa haya yanaarifiwa na vyombo vya habari na magazeti ya ndani, jambo ambalo linatia mkazo kwamba tunaishi katika hali ya hatari yenye kutisha, na ni wajibu tutangaze sote hali ya hatari na tuangalie upya utamaduni wetu na mfumo wetu wa mafundisho yetu, na vile vile utekelezaji wa vyombo vya usalama na mahakama. Hali hii inazidi kuongezeka katika jamii yetu, nilimuuliza mmoja wa viongozi katika upande husika je yanayotangazwa katika majarida ni jambo lililotiwa chumvi? Akanijibu: “Bali yanayotangazwa ni sehemu ndogo tu katika yanayotokea katika jamii.”

Na taarifa za kimataifa zinaashiria kwamba nchi bora zaidi katika ulimwenguiliyofaulu kupu

Utafiti unasema: Sababu ni wingi wa taasisi za vijana Japan, ambapo kuna taasisi 540 elfu zinazojali vijana, moja ya taasisi hizo jina lake ni Umoja wa Vijana wa Uongozaji na Uelekezaji, katika umoja huo kuna vijana 126 elfu wenye kujitolea miongoni mwa vijana, na kuna taasisi za wanawake za uwezeshaji zinazohusika na wanawake tu, na humo kuna wanawake 360 wenye kujitolea.

Uwepo wa taasisi ambazo zinashughulika na vijana na kuwavutia ni jambo la dharura, na linalosaidia kupunguza ongezeko la makosa katika jamii. Na ni wajibu wetu kutumia fursa ya uwepo wa vijana katika majilisi za Husein ili kuwaelekeza vijana na kuhamasisha jamii kuwa na mfano wa taasisi kama hizi. Kama ambavyo ni wajibu wetu tusifurahie sana mengi yanayotokea katika Ashura katika kuamiliana na maadhimisho, ikiwa tu hatujayatumia katika kurekebisha nyendo za kijamii, hakika kuamiliana huku kunatubebesha jukumu kubwanalo ni kutoghafilika na yanayotokea katika jamii, kila mmoja ni mwenye jukumu, na vyombo vya usalama vina jukumu lake navyo vinatakiwa vitoe juhudi za ziada, ni sahihi kwamba vinashughulika na kupambana na ugaidi, lakini wananchi wanatarajia dauru kubwa zaidi katika kulinda amaniya jamii, na upande wa mahakama vilevike ni juu yake uwe mkali zaidi katika kutoa hukumu, kwa sababu wapuuzi (waovu)wanapohisi kuwepo kwa ulaini hakika hilo linawasukumakufanya makosa na kutojaliadhabu. Inapasa onyo liwe kwa kiwango kinachotakiwa ambacho anastahili muovu, na sio kuwa laini kwa wakosaji na kuruhusu misamaha, kwani sisi tuko katika kipindi ambacho tunahitaji ukali.