Change Language: English

ASHURA:SIKU YA HUZUNI KUBWA NA ZINDUKO KWA UISLAMU WA SHI’A

Mtu amesimama peke yake katika jangwa, akiwa amebeba kichanga chake cha kiume
kifuani. Wafuasi wake, ndugu yake na watoto wake wa kiume wote sasa wamekufa,
isipokuwa mwanawe mkubwa ambaye amalala kwenye hema lao lililopasuliwa akiwa
mgonjwa mahututi. Hajapata funda ya maji kwa siku tatu mfululizo, tangu yule
dhalimu Yazid alipoamuru familia yake wakoseshwe chakula au wauawe.

Anapaza sauti akilalamika: “Hivi hakuna kati yenu ambaye ana watoto wa kuwazaa mwenyewe?
Mnaweza kuonyesha huruma kwa mwanangu huyu, na mkampatia japo funda moja ya
maji? Majibu yalikuwa ni mshale ambao ulichana shingo ya mtoto huyo mchanga!

Ashura ni kisa cha Imam Hussein (a.s) ambaye aliuwawa Shahid na majeshi ya Yazid katika
mawanda ya Karbala ndani ya Iraqi ya sasa. Neno “Ashura” lina maana ya“ya 10” kwa vile inaangukia katika siku ya 10
ya Muharram katika kalenda ya Kiislamu. Kadhia ya Imam Hussein (a.s) ni tukio
la muhanga, na mzinduko ili kuukataa katakata udhalimu na kuhifadhi maadili ya
jamii na thamani ya dini ya Uislam kutokana na upotovu.

Khalifa mwenye imani za kianasa, Yazid, akitawala kutoka Damascus, alitaka kumlazimisha
Imam Hussein (a.s) kutoa kiapo cha utii kwake, ili kupata uhalali wa madai yake
ya mamlaka ya kiroho na kisiasa.

Hussein (a.s) alikuwa ni mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mtoto na Khalifa wa nne,
Ali bin Abi Talib (SA) (Ufupisho wa AS unasimama mahali pa “Alayhis Salaam”
ambayo kwa desturi inatumeka kiheshima kwa majina ya watu mashuhuri katika
Uislam. Hii akronimi SAW ni kufupi cha maneno kama hicho ambacho kinatumika kwa
Mtukufu Mtume Muhammad peke yake, ambacho kinatafsirika “Rehma na amani juu
yake”).

Yazid alijua kwamba utawala wake ulitegemea juu ya kupata kiapo cha utii cha Hussein (a.s).
Hussein (a.s) hakutafuta mamlaka ya kisiasa kwa ajili yake au kuchukua mahali
pa Yazid. Hussein (a.s) alitaka tu kuteteamamlaka yake ya kiroho na kuwaongoza Waislamu katika dini. Lakini mamlaka yakeya kiroho yalichukuliwa kama tishio la kisiasa na Yazid, na kukataa kwake kutii amri kama ni kitendo cha Uasi. Umuhimu wa Ashura kwa Waislamu wa Shi’a ni
katika kuomboleza mauwaji ya Hussein (a.s), bali pia katika kuzinduka kwa ajili
ya kufanya kilicho haki na sawa kwa ajili ya wema na manufaa makubwa zaidi.
Muhanga wa Hussein (a.s) unatukumbusha sisi kwamba tusizipatie nafasi nguvu au
majeshi ambayo yanataka kushirikisha dini kwa maslahi ya kisiasa, kwa hiyo tusitelekeze
maadili na ithkadi zetu.

Ashura sio mafundisho ya kimadhehebu bali ni ujumbe usio na wakati ambao unavuma katika
kila zama. Waislamu leo hii (Shi’a na wasio Shi’a) wanaweza kupata mzinduko
kutoka kwa Hussein (a.s) kwa namna nyingi, kama vile kuchagua kushikilia kile
kinachoitwa “Vazi la Uislamu” (la hofu na mshangao wa Juan William) licha ya
nadhani isiyotakikana inayoweza kuwasababishia. Kadhalika, ndani ya Yazid
tunaweza kuona nyuso za madhalimu wengine mwote katika historia ambao wameiita
na kuipotosha dini katika kuendeleza tamaa zao za kisiasa zilizo tupu kabisa.

Lakini maana kuu ya Ashura lazima iwe ni huzuni. Kuna msiba mkubwa sana katika kifo cha
Kishahidi cha mtu mtakatifu, na Hussein (a.s) alikuwa ni fahari (Prince)
miongo mwa watakatifu. Waislamu wa Shi’a wanaadhimisha tukio la Ashura kwa
kusoma marathiya, visomo vyenye mahadhi ambavyo vinahadithia ile kadhia
ya Karbala. Vile vile sisi tunaonyesha kwa ishara huzuni zetu kwa matam,
yaani ishara ya upigaji vifua vyetu kwa viganja vyetu vya wazi. Kaida hizi
zinafanywa ndani ya majlis, yaani mkusanyiko wa watu ndani ya miskiti au vituo
vinginevyo, katika siku zinazoelekea kwenye Ashura na mnamo siku yenyewe ya
Ashura. Hivyo Waislamu wa Shi’a wameadhimisha na kukumbuka muhanaga waHussein (a.s) kwa karne nyingi sasa.

Katika huzuni yetu ndimo mna wajibu wetu wa kutimiza ile amana isiyokamilika iliyowekwa
juu yetu naImam Hussein (a.s). Yeye
Hussein (a.s) alilala kuegemea kwenye mti, akiwa amepigwa na kumwagwa damu, kachanwa
chanwa kwa mishale na panga. Yule mwovu Shimr (kutoka kwenye jeshi la Yazid)
alimjia na kisha akamsukumiza kwa nguvu ardhini. Shimr huyu akakaa juu ya kifua
cha Hussein (a.s) na akajaribu kukata shingo yake kwa kisu butu.

Kwa nguvu za ghafla, Hussein (a.s) akamtupa Shimr kutoka kifuani mwake, na kisha akafanya
Sajda moja ya mwisho. Katika kitambo kile cha mwisho cha mpito, kabla Shimr
hajashusha upanga wake, du’a ilisikika kutoka kwake Hussein (a.s).

SIKU YA ASHURA - MWEZI 10 MUHARRAM – KALENDA YA KIISLAM.