NI BAYANA KAMA ANGA
Utangulizi: Wamesema kuhusu Husein Ni rahisi mno kwa mtu yeyote kuandika kuhusu tukio ambalo analiona au kusoma au kusikia kuhusu tukio hilo, hasa kama kuna uwezekano wa tukio hilo kushika nafasi wakati wowote na popote. Na taarifa kuhusu tukio hilo na wahusika katika
tukio hilo, wakati mwingine inakuwa ni mada kuu kwa mtu kuandika kuhusu ambacho
kimetokea na sifa za wahusika, kama mtu huyo ni mtunzi au mshairi au ana sifa
zote mbili (mtunzi na mshairi). Basi, watunzi wa wakati huu wameacha mamia au
maelfu ya matukio ya historia zinazoendana na vita, polisi, jamii, upendo na mifano mingine kama hii.
Lakini mjadala juu ya tukio la Karbala na kufa kishahidi kwa Imam Husein (a.s) na familia yake katika siku ya Ashura, mwaka wa 61 Hijiria, sio tukio lililofichika. Kwa hiyo, mjadala juu ya hili hauna ukomo wa mtu mmoja au siku moja tu.
Kwa kweli, tukio hili linaanzia kwa kuondoka Imam Husein (a.s) kutoka Madina kwenda
Makka, kisha kutoka Makka kwenda Karbala, safari iliyokusanya mabonde na vituo
kumi, na kisha safari ya familia yake kutoka Karbala kwenda Kufa, na kutoka
Kufa kwenda Syria, wakitembea kupitia nchi namiji kadhaa mikubwa, na kisha kurudi kwao toka Syria na kuelekea Karbala, na kisha kwenda Madina, na kisha kuenea kwa ujumbe wa Karbalakaribu dunia nzima.
Tukio la Karbala pia linahusisha wakati wa kukamilika ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), tangu mwaka wa 12 Hijiria, ambao unaendelea mpaka sasa na utaendelea kubakia mpaka mwisho wa dunia. Hakika, tukio la Karbala limeenea duniani kote kila muda na kila sehemu, na hivyo sio kosa kusema kwamba kuandika kuhusu tukio hili ni
sawa na bahari ambayo haijulikani kina chake, kwa sababu Imam Husein (a.s) sio
tu kiongozi kwa ajili ya Waislamu lakini ni kiongozi kwa ajili ya kila binadamu.
Harakati yake haikomei tu wala kuhusishwa tu na harakati ya Uislamu uliyotambulishwa
na babu yake Mtume Muhammad (s.a.w.w), na yeye (a.s) si mrithi wa baba yake tu Imam Ali (a.s), au kaka yake tu Imam Hassan (a.s), kwa kuhusisha Uimamu, bali kwa hakika yeye ni mrithi wa Mitume wote na wajumbe wote kuanzia Mtume wa kwanza Adam (a.s)mpaka Mtumewa mwisho Muhammad (s.a.w.w). Kwa hiyo, ni kiongozi wa kila Mwislamu na wasiokuwa Waislamu, na ni rehema kwa wanadamu wote. Na ni kiongozi wa mashahidi kuanzia wa mwanzo hadi wa mwisho.
Mchango wa Imam Husein (a.s) na athari zake vinahitajika kushikiliwa katika kila
ustaarabu, na kila lugha izungumzwayo katika dunia ni lazima isisahaulike. Nimechukua
juhudi za kufanya hili jepesi kutoka katika Inklopedia ya Husein iliyoandikwa
na Ayatollah Dokta Mohammad Sadiq Al-Karbasi, ambayo ni mafanikio makubwa
katika historia ya uandishi juu ya Imam Husein (a.s) ulimwenguni, ambayo imefikia
juzuu 750 na leo ni zaidi ya juzuu 80 zimechapishwa ambazo zimebeba zaidi ya
milango 60 kuanzia kwenye maisha ya Imam Husein (a.s), na hii ndio sifa ya
pekee ya Inklopedia ya Imam Husain ambayo mtunzi alianza kuiandika mwaka 1987 kwamba inazungumzia mada moja tu,
“Mchango wa Imam Husein a.s”, na hii idadi kubwa ya juzuu za kitabu hicho kihakika ni ili kueneza nuru ya utu wa Imam Husein a.s, ambao kiukweli ni kigezo cha kufuatwa na kila Taifa ili kufikia manufaa, umakini, na kupata uhuru kutokana na maovu ya ukandamizwaji na wakandamizaji. Kama ilivyoeleweka kwamba mchango wa Imam Husein a.s ni muhimu sana katika jamii ya maisha ya mwanadamu, tumeona kila taifa limechukua mafundisho ya Imam Husein (a.s) kama mfano katika maisha yao.
Kuanzia hapa, Inklopedia ya Husein inaelezea kuhusu mchango wa Imam Husein (a.s) katika lugha zote ulimwenguni, ingawa kiarabu pekee ndio lugha kuu lakini imekusanya
lugha zote, mfano mtunzi ameandika kuhusu fasihi ya Imam Husein a.s kwenye
fasihi ya Urdu, Pashto, Kiingereza, Kiajemi, na lugha nyingine, na hili ndilo lililopelekea
Inklopedia ya Husein kupata heshima kubwa ulimwenguni kati ya Inklopedia nyingine,
na Inklopedia hii iko juu pindi linapojitokeza jambo la utafiti na mjadala kuhusiana naye na pia kuhusiana na mada yenye uhusiano naye.
Kivitendo, Imam Husein (as) amebeba nuru ya ushindi na inaweza kuonekana katika mwenendo mzima wa kuelekea kwenye amani na rehema kwa kila taifa, na hii ni nuru ambayo kila kiongozi ulimwenguni kutoka imani na mataifa mbalimbali amekuwa akifuata nyayo za Imam Husein (a.s)na kuangazia harakati zake kwa nuru ya Imam Husein a.s kwa kuwavutia watu kuelekea katika amani.
Hili ni kubwa mno kutoka kwa Dokta Karbis pindi alipojumuisha katika Inklopedia yake
mlango wa kile kilichokuwa kikijadiliwa kuhusu Imam Husein (a.s) na watu wenye mila
na tamaduni za wasio Waislamu, na umeitwa “Wamesema kuhusu Imam Husein a.s.” na kwa kuendelea kupitia juzuu hii nimeona watu mashuhuri kutoka mataifa na dini mbalimbali wakitoa mawazo yao kuhusu Imam Husein (a.s) na kutangaza upendo na mapenzi kwake. Huu ni moja ya ushahidi mzito kuhusu Imam Husein (a.s.) kuwa utu wake ni kwa ajili ya kila kundi la fikra, sio tu kwa ajili ya Waislamu, bali ujumbe wa Imam Husein umeenea kwenye moyo wa mataifayote kama damu inavyoenea katika mishipa.
Na nimemuona Sheikh Karbasi amejumuisha maadili yasemwayo kuhusu Imam Husein (a.s.) na kwa hakika ni mtazamo wa maadili tu ndio unaoweza kudhihirishwa na utu wenye maadili.
Hii ni bora mno kwa Sheikh Karbasi pindi anapoandika utangulizi wa sura hii pamoja na utafiti wake kwamba kila msemo uliotolewa kuhusu utukufu na wasifu wa Imam Husein (a.s.) ameuweka pamoja na asili yake, chanzo na rejea yake, na kwa sababu hii ni kwa mara ya kwanza katika historia nimeona kitabu chenye taarifa za ndani zaidi kuhusu mada hii sambamba na maandiko na ufafanuzi wake na undani wa wasifu wa yule aliyesema maneno husika.
Sheikh Karbasi ameleta mwelekeo mpya wa uwasilishaji ambao huwezi kuuona katika vitabu vingine na hili linatupa dhana ya jumla kuhusu Inklopedia ya Imam Husein kuwa ni usomi wa kikweli na utambulisho wa mlolongo wa vitabu wenye nia ya kueneza taarifa kuhusu Imam Husein (a.s) ambao unaweza kuwa na manufaa kwa wasomaji, waandishi, watafiti, na wajadili. Na pia amewasilisha kazi ya utafiti wake kwa nyenzo ya mkono na chanzo cha udondoaji wa taarifa kwa ajili ya watafiti hasa juu ya mada hii na mada nyingine kwa ujumla.
Ukweli ni kwamba hakuna Inklopedia kama hii inayoelezea kuhusu Imam Husein (as) kwa kiwango hiki cha taarifa, iwe fupi au ndefu, hiyo utaiona katika Inklopedia ya Imam Husein (as) iliyoandikwa na Dokta Karbasi ambaye ni mtunzi, mtafiti, mwanafiqhi, mwanachuoni, mwanafasihi, mshairi, na kwa hakika ni mwanachuoni mkubwa wa kidini, na Inklopedia yake iko bayana kama anga.