Change Language: English

Utaratibu makini (Formula) wa Imamu Husein (a.s)

Imamu Husein (a.s) aliandika:

“Siondoki (Madina) kama muasi, mkandamizaji na mchupa mipaka, bali madhumuni yangu ni kuutemgeneza Umma wa babu yangu. Njia pekee ya kufanya mageuzi haya ni kwa Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu. Nataka kupita njia aliyopita babu yangu na baba yangu Ali bin Abu Talib.”

Yaani nataka kuutengeneza Umma kwa njia ya Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu. Huu ni msemo wa aina ya pekee wa Imamu Husein (as) kwa sababu maneno mengi mengine ya Imamu (as) yako katika mtindo wa hutuba, lakini haya ni maneno ambayo aliyatoa kwa maandishi. Huu ulikuwa ni utaratibu makini uliotolewa kwa jamii zilizokufa na mtabibu wa Umma juu ya jinsi ya kuhuisha mataifa (Umma) yaliyokufa.

Anasema “Siondoki kwenda kusababisha ufisadi au uovu” au kwa lugha ya kisasa, alikuwa anasema kwamba sikuja kufanya unyang’anyi na vurugu mitaani, kuvunja vioo na kuchoma mipira ya magari. “Naondoka kwenda kuutengeneza Umma wa babu yangu…” Nukta ya kutazamwa hapa ni kwamba mageuzi (utengenezaji) hufanywa tu juu ya vitu ambavyo vina kasoro au vimefisidi; hayafanywi juu ya vitu vinavyofanya kazi vizuri. Imamu Husein (as) hasemi kwamba ninakwenda kufanya mageuzi juu ya Yazid bali badala yake anasema kwamba naondoka kwa ajili ya kuutengeneza Umma. Tunahitaji kutafakari hapa kwamba Yazid alikuwa fisadi muovu, basi kwa nini Imamu (as) anaondoka kwa ajili ya kuutengeneza Umma? Huyu (as) ni tabibu wa aina gani?

Kuna kisa kidogo ambacho tumezoea kukisikiliza kutoka kwa wazee wetu katika umri wetu wa ujana, ambacho siwezi kukielewa kwa wakati huu. Mara mgonjwa anapokwenda kumuona daktari akilalamika kuhusu maumivu ya tumbo; daktari humuuliza chakula alichokula usiku wa jana. Hujibu kwamba alikula chakula cha kawaida ambacho ni mkate, lakini ulikuwa umeungua kidogo na haukuiva vizuri. Daktari anamuambia alale kitandani na afungue macho yake ili amuweke dawa ya matone machoni, lakini mgonjwa anakataa. Daktari huyu alikuwa mtu mwenye busara ambaye alitambua sababu ya maumivu ya tumbo lake, ambayo ilikuwa ni kwa sababu ya matatizo ya kutoona vizuri. Kama angekuwa na nuru nzuri ya macho basi angelitambua kwamba mkate ule ulikuwa umeungua na haukuiva vizuri na hivyo asingeula na asingepata maumivu ya tumbo. Daktari alimwambia kwamba kama nikikupa dawa ya kuponya maumivu yako ya tumbo itakuponya leo lakini tena kesho utakula mkate ambao haukuiva vizuri na utakuja tena na tatizo hili hili. Kwa hiyo, kwanza nuru yako ya macho inahitaji matibabu ili macho yako yaweze kutambua chakula kichafu na kilichooza ambacho husababisha matatizo ya tumbo. Hivyo, kama upugufu wa nuru katika macho ya mtu unaweza kusababisha maumivu ya tumbo, basi ukosefu wa visheni (uoni) wa jamii utasababisha maumivu na ufisadi katika jamii nzima. Ukosefu huu wa visheni ni ule wa Umma, hivyo Imamu (as) alisema ninakwenda kurekebisha visheni hii kwa kuutengeneza Umma. Yazid alikwa fisadi na uovu wake umefikia kiasi ambacho hawezi kurekebishwa, lakini tatizo halikuwa Yazid kama Yazid ilikuwa ni u-Yazid ambao ungekuja kuwepo zama yoyote, na u-Yazid unaweza tu kuangamizwa kama Umma ungeweza kuwa na uoni wa kuutambua. Kama Umma haukujenga visheni hii, Yazid ibn Mu’awiya mmoja atatoweka lakini mtoto wa mtu mwingine atajitokeza kama Yazid. Yazid huenda anaweza akatokea baada ya miaka elfu moja na mia nne; na kwa hiyo kazi yangu sio kummaliza Yazid mmoja bali Mayazid wa zama zote.

Ni ufisadi gani uliokuwepo katika Umma? Walikuwa walevi, wazinifu, wezi au majambazi? Hii haikuwa sababu kama inavyoonekana kwenye kumbukumbu za kihistoria kama ushahidi, wakati Kiongozi wa Mashahidi (as) alipoondoka Makka Umma haukuwa unajishighulisha na ulevi wa pombe, walikuwa wakijishughulisha na ibada za Hijja; halikadhalika wakati alipoondoka Madina Umma haukuwa umejitumbukiza katika unywaji wa pombe, bali walikuwa wamejishughulisha na Ziarat ya kaburi la Mtukufu Mtume (saw). “Ewe Aba Abdillah (Husein)! Unasema kwamba unatoka kwa ajili ya kuutengeneza Umma, lakini Umma huu uko katika kushughulika na Hijja, Ziarat ya kaburi la Mtume na ibada mbalimbali, hivyo ni matengenezo (mageuzi) ya aina gani unayopanga kwa ajili ya Umma huu ambao unaonekana kuwa na mageuzi tayari? Yeye (as) anasema ufisadi mmoja mkubwa umeibuka katika jamii hii. Ni ufisadi gani huo? Mtu kama Yazid amechukua madaraka, amekaa juu ya vichwa vyao, amenyakua madaraka ya utawala na kisha ametangaza Halali kama Haramu na Haramu kama Halali, amevuka mipaka ya Uislamu na pamoja na yote haya yanayotokea mbele ya Umma bado Umma hautanabahi. Maradhi ambayo Umma huu umeyapata ni yale ya kupumbaa na kutokujali. Niliwaambia kuvua Ihram zao (mavazi ya Hijja), lakini walikuwa wana hamasa zaidi kuhusu ibada (hiyo ya Hijja) kiasi kwamba walimuacha Imamu wa Umma akiwa ametengwa kwa ajili ya ibada. Walikuwa na mipango ya kukaa Mina, Arafa ili kupata malipo (Thawaab), kisha wachinje wanyama wao huko Mina na kwa dhabihu hizo wafanye shughuli za ustawi wa jamii. Hata leo Umma una hamu ya juu sana ya kufanya shughuli za ustawi wa kijamii kama ilivyokuwa zama hizo, na kama kwa matokeo ya hamasa yao kuhusu ibada (zisizo za kiroho) na ustawi wa kijamii wanakuwa wazembe, wasio na hisia na kutokujali kuhusu mtu kama Yazid kuwa kiongozi wao. Hivyo ufisadi wa Umma hauna maana kwao na kutokuwa huku na maana ni kifo cha Umma na jamii.

“Ewe Aba Abdallah! Hivyo vipi utauamsha Umma huu? Yeye (as) alisema:

“Nimekusudia kufanya kuamrisha mema na kukataza maovu.

Hii ni kwa sababu kinachosababisha kifo cha jamii ni ni kuacha kufanya Kuamrisha Mema na Kukataza Maovu. Nataka kuihuisha jamii hii iliyokufa kwa kufanya matendo haya. Kuamrisha Mema ni nini? Haina maana ya kuvaa suruali fupi, kufuga ndevu au kukaa kwa adabu, kufanya matendo fulani ukielekea Mashariki au Magharibi au kuhoji watu kuhusu mtindo wao wa kuongea. Kuamrisha Mema ni kuufanya Umma usiojali wawe wenye kujali kuhusu mambo ya jamii; ni kujenga hisia katika Umma usio na hisia. Ni kuwaleta watazamaji kutoka nje ya uwanja wa michezo na kuwaingiza kwenye uwanja. Uovu mkubwa ni kuwa wapumbavu wasio na hisia, na hili lilitangazwa na Kiongozi wa Mashahidi (as) kama uovu mkubwa, wakati ambapo alisema:

Je, hamuoni kwamba haki haitekelezwi, hamuoni kwamba batili haikatazwi? (Musawate Kalemate Imam Hussain (a.s) – uk. 356)

Imamu (as) alikuwa anawaambia kwamba mmekuwa vipofu; hamuwezi kuona kwamba haki inavunjwa na ninyi mmekaa kama watazamaji walio kimya. Huu ulikuwa uovu mkubwa kwamba watu wamekuwa wazembe, bila hisia na watazamaji wakimya kwenye udhalimu. Ukosefu huu wa hisia unaweza kufikia kiasi kwamba mjukuu wa Mtume (saw) anauliwa kishahidi pale Karbala na watu hawa walikuwa wanaangalia kama watazamaji wakiwa wamekaa mjini Kufa. Na wale mateka ambao waliachwa nyuma kule Karbala, wakati walipowasili Kufa watazamaji hawa walionesha tu huzuni zao kwao na kuomboleza. Na sasa, baada ya harakati za mwana wa Zahra (as) ilikuwa ni zamu ya Binti wa Zahra (as) kuendeleza harakati hizi kuanzia hapa.

Alitoa hotuba akielezea kwamba ninyi ni wahaini, wasaliti na watazamaji ambao wamekaa kwenye uwanja wa michezo na kuonesha huzuni kwa mateka na kuombeleza juu ya mashahidi wa Karbala. Haki gani wanayo watazamaji kama ninyi ya kuomboleza juu ya watu wa Karbala? Dhuria wa Mtume (as) wanauliwa na kuwa wafungwa, na watazamaji hawa wakimya walikuwa wanaangalia tu wakiishia kwenye kuomboleza. Hawa walikuwa watu ambao kwamba Bibi Zainab (as) aliwahutubia na akasema:

Mnamlilia kaka yangu? Mnastahili kulia, na lieni sana!

Ni nani aliyekuwa anawaambia maneno haya? Ni kwa wale waliokuwa wanaomboleza kwa ajili ya kaka yake. Kama leo vilevile tunasema kwamba Bibi Zainab (as) ilikuwa inamhusu iwapo watakuwepo watu watakaomlilia kaka yake. Wahadhiri wetu wanasema kwamba ilikuwa hamu ya Bibi Zainab (as) kuona watu wanamlilia kaka yake. Hivyo hamu hiyo imetimizwa kwa muda wa siku mbili tu kupita, Imamu Husein (as) aliuawa mwezi 10 Muharram na mwezi 12 Muharram walikuwepo watu wanaoomboleza kifo chake katika mji wa Kufa mbele kabisa ya Bibi Zainab. Lakini alisema hataki macho haya yanayolia na alichukia. Hii ni kwa sababu alikuwa anawaambia kwamba vichwa vya familia yetu na masahaba viko juu ya mikuki na ninyi mnaomboleza juu ya hili? Hiki ndio kiasi cha wajibu wenu cha kuangalia tu vichwa juu ya mikuki na kulia kama watazamaji? Kama mnataka kuomboleza kwanza jitokezeni mbele na kuchangia kwenye vichwa juu ya mikuki, na ninyi mikono yenu ifungwe, ifungwe minyororo shingoni mwenu kwanza, angalau fanya kitu kwanza na kisha njoo ulie. Kama unataka kweli kuomboleza basi njooni upande wetu na ombolezeni, msiwe upande mwingine kama watazamaji.

Vipi ukimya huu juu ya Umma usiojali na usio na hisia utakavyovunjwa? Ni kwa vifo hivi vya kishahidi kwamba Kiongozi wa Mashahidi (as) alipuliza uhai katika jamii. Mwana wa Zahra (as), mrithi wa fahari ya Masihi aliihuisha jamii hii. Na chochote kilichoachwa katika kazi hii kilikamilishwa na dada yake, Bibi Zainab (as). Hii ndio sababu mtu huyu mkubwa Imamu Khomein (r.a) alisema:

“Uislamu ni jina la sifa mbili tu; imma sifa ya Husein (as) au sifa ya Zainab (as).”

Ina maana kwamba amma fanya majukumu yako kwa damu au beba ujumbe wa mashahidi kama Zainab (as) kwenda kila mtaa na kona; hivyo amma uwe kama Husein au Zainab (as). Kama wewe sio kama Husein au Zainab, basi wewe ni mtu wa mji wa Kufa (watazamaji wakimya wasiojali). Na chochote afanyacho mtu wa Kufa hakitakiwi na Ahlul Bayt (as). Hawataki maombolezo yao na hata tabasamu zao, hawataki mikusanyiko ya wa-Kufa na wala ibada zao. Ahlu Bayt (as) hawategemei chochote kutoka kwetu bali kuwa wa-Huseini na wa-Zainab. Amma lazima tutoe damu katika njia hii au kujitokeza kutetea na kulinda damu ya mashahidi hawa.

Ninayasema haya kwa familia za Mashahidi kwamba lazima muwe na fahari ya jambo hili kwamba mmetoa mashahidi katika njia ya dini. Lakini kuwa Shahidi na kuunyweshea mti wa dini kwa damu bado ni rahisi. Hatua mpaka Karbala ilikuwa bado ni rahisi lakini jukumu la Zainab (as) lilikuwa gumu sana. Mashahidi hawa wa Pakistan wametembea juu ya njia ya mwana wa Zahra (as) lakini wale ambao wako hai na wapo sasa lazima wawe na sifa ya Zahra (as), na hii ni njia ngumu sana. Hili ni jukumu gumu mno kiasi kwamba Sayyidus Sajidin (as) alilazimika kulia katika kila hali. Yeye (as) hakuomboleza kule Karbala; wakati wote alipokuwa anaulizwa kuhusu hali inayomuumiza sana, kamwe hajasema Karbala; siku zote alisema “Sham” (Damascus). Hii ni kwa sababu kuanzia mwanzo mpaka Karbala ulikuwa ni uwanja wa Husein (as), lakini kwa Bibi Zainab (as) “Sham” (Damascus) ilikuwa ni uwanja wake. Ili kuwa mrithi wa mashahidi, uaminifu wa Bibi Zainab (as) na kutetea madhumuni ya mashahidi ni vigumu sana; kwa kiasi kwamba ilimfanya Imamu Sajjad (as) aomboleze maisha yake yote. Ni jukumu la Bibi Zainab; yaani misiba kamili na hivyo ni vigumu sana.

Jukumu la jamaa wa familia wa mashahidi wa leo sio kudai na kukusanya fidia kutoka serikalini kwa ajili ya miili ya mashahidi. Hii ni kwa sababu wakati Yazid alipomuuliza Imamu Sajjad (as) kumjulisha kuhusu fidia kwa ajili ya hasara iliyopatikana kule Karbala; Imamu (as) alisema ni vipi hasara hii itafidiwa?

Nilihuzunika sana wakati niliposikia kwamba madai katika maandamano yaliyoandaliwa kwa ajili ya Mashahidi katika mji mmoja yalikuwa kwamba fidia kwa ajili ya Mashahidi hawa lazima iwe sawa na ile iliyotolewa katika mji mwingine wakati fulani huko nyuma. Huu ni wakati ambapo lazima tujibu kama Imamu Sajjad (as): “Ewe maalun! Je, unajua hasara uliyosababisha? Je, unajua ulichochukua kutoka kwetu? Hutaweza kuelewa thamani ya hasara ya maisha haya yaliyopotea.” Leo vilevile lazima tuwajibu Mayazid wa zama zetu kwa sauti ileile wakati wao wanapozungumza kuhusu kufidia hasara ya miili hii. Lazima tuwaambie; ni kitu gani mlichonacho ambacho mnaweza kufidia Mashahidi hawa? Kwa jina la Allah (s) huwezi kufidia hata kucha ya kidole cha mmoja wa Mashahidi hawa.

Mwanafasihi mmoja wa Iran aliwasilisha cheo cha Bibi Zainab (as) katika hali nzuri na ya kupendeza; anasema:

“Karbala ingekufa kama Zainab (as) asingekuwepo kule. Ushia ungetoweka kama Zainab (as) asingekuwepo.”

Kama Karbala iko hai ni kwa sababu ya juhudi kubwa za huyu Bibi Zainab (as). Leo kila mmoja anazungumzia kuhusu fidia na ustawi wa familia za Mashahidi, lakini watu wanapuuza madhumuni ya kufa kishahidi. Bibi Zainab (as) amekuwa mlezi wa mayatima, lakini vilevile aliwasilisha madhumuni ya kufa kishahidi kwa ulimwengu. Leo familia za Mashahidi lazima vilevile zifanye hivyo hivyo na kuwajibu Mayazid wa nchi yetu (zetu) kwa sauti ileile ya Zainab (as) na Imamu Sajjad (as).