Change Language: English

Ukweli wa Maisha na Kifo

Falsafa ya Kifo cha ki-Shahidi kama ilivyotajwa katika maneno ya kiungu na Qur’ani Tukufu ambayo Maasumin Watukufu (as) wametafsiri na kuielezea kwetu katika uhalisia ni Falsafa ya dini na Uislamu. Mwanadamu ambaye anaweza kuelewa uhalisia wa kifo cha ki-Shahidi ni mdai wa kweli wa uelewaji wa uhalisia wa dini au angalau amekuwa imara katika uelewaji wa uhalisia wa dini. Lakini kwa watu wa kawaida kama sisi ambao hatuelewi hata uhalisia wa kifo ni vigumu kwetu kuelewa uhalisia wa kifo cha ki-Shahidi. Huu ni ukweli kwamba hatuna ujuzi kuhusu uhalisia wa kifo kwa sababu maisha yetu ni ushahidi kwamba hatuna habari kuhusu siri na uhalisia nyuma ya kifo. Ili kuelewa maana ya maisha, mwanadamu kwanza anahitaji kuelewa kifo kwa sababu kifo ndicho kinachotoa maana ya maisha. Kama siri ya kifo ikidhihirika katika maana yake ya kweli basi wale ambao wanaogopa kifo watabadilika kuwa wapenzi wake. Ni kwa sababu ya kifo kwamba maisha ni mwendo kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, na tulipitia kwenye kifo kilichopita kabla ya kuingia katika ulimwengu huu. Tumefikia kwenye uhai huu kwa sababu ya vifo mbalimbali, kama tusingekufa kabla tusingekuwa hai leo. Lugha ya Urdu inaelezea kifo katika njia nzuri sana ukilinganisha na lugha nyingine. Katika Urdu kifo kimetajwa kama “Inteqal,” neno ambalo humaanisha mwendo. Mwanadamu hupiga mwendo kwa sababu ya kifo, kwa hiyo kifo sio mwisho; ni mwendo kutoka hali moja kwenda kwenye hali nyingine. Tulikuwa katika hali moja kabla ya kuzaliwa na kisha tulikuja kwenye hali hii ya maisha na kuicha hali ile nyuma. Ilikuwa ni kifo cha hali ya kwanza ambacho kimetuleta kwenye maisha katika hali hii.

Sisi ni waathirika wa kutokuelewa kwingi ambako Qur’ani Tukufu imerekebisha. Tuna mawazo mengi yasio sahihi, fikra na uelewaji katika akili zetu; na tunatumia maisha yetu yote chini ya kivuli cha fikra na uelewaji huu usio sahihi. Qur’ani imebatilisha upotoshaji mwingi kama huo ambao ungetupeleka kwenye maangamizi. Kwa mfano, migogoro mingi kati ya majirani na jamaa wa familia ni kwa sababu ya mambo madogo tu ya kutokuelewana. Kama kutokuelewana huku kunaondolewa basi migogoro hii pia itatatuliwa. Mwanadamu hujenga picha isiyo sahihi kuhusu mtu fulani, kisha mawazo haya yasiyo sahihi yanakuzwa na kugeuka kuwa migogoro na matokeo yake ni kutengana kwa marafiki, ndugu, jamaa wa familia, waumini na Waislamu. Qur’ani Tukufu imefanya maandalizi mahususi ili kurekebisha kutokuelewa, kwa sababu kutokuelewa huku kutaangamiza na kuuwa wanadamu. Miongoni mwa kutokuelewa huku ni kutokuelewa kuhusu kifo na maisha. Tunakichukulia kifo kama maangamizi wakati ambapo kula, kunywa kutembea na uzazi huchukuliwa kama maisha. Ukuaji wa daraja hii ya juu ya kutokuelewa ndani ya mwanadamu unaweza kusababisha maangamizi yake mwenyewe. Qur’ani Tukufu imesahihisha kwamba maisha hayana maana ya kula na kunywa; na wala kifo sio mwisho wa mapigo ya moyo. Qur’ani huchukulia watu wengi wanaoishi, kutembea, kuzungumza na kula kama wafu, wakati ambapo tumeamrishwa na Qur’ani kuwachukulia watu wengi waliokufa kuwa wako hai. Hivyo tunajua kwamba tuna kutokuelewa kubaya mno kuhusu kifo na maisha. Qur’ani Tukufu imefafanua kwamba hatupaswi kuwachukulia wale ambao shingo zao zimekatwa, ambao vifua vyao vimepasuliwa kwa risasi na ambao mapigo yao ya moyo yamesimama kama wafu. Kiuhalisia wakati tukiona watu katika hali kama hiyo mara moja huwaita kama wafu ambako Qur’ani hujitokeza na papohapo pamoja na msemo:

Wala usiwe na mashaka, ni lini hawa walikuwa wafu na lini wale ambao wanatembea wakiwa hai?

Hivyo kwanza lazima tuelewe maana halisi ya maisha, kisha ni hapo tu ndipo tutaelewa kifo na baada ya hili tutambua maana ya kifo cha ki-Shahidi.