Change Language: English

Mwezi mtukufu wa Muharram

Muharram ni mwezi wa kwanza (mwandamo) wa kalenda ya Kiislamu.

Mwenyezi Mungu, anasema:

“Idadi ya Miezi mbele ya Mwenyezi Mungu ni kumi na miwili kwa ilimu ya Mwenyezi Mungu siku Alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo imo minne mitukufu kabisa. Hiyo ndiyo dini iliyo sawa. Basi msijidhulumu nafsi zenu katika (miezi) hiyo.” (9:36)

Huu ni mmoja kati ya miezi minne mitukufu iliyotajwa ndani ya Qur’an, mingine ikiwa ni Rajab, (Mwezi wa 7), Dhul Qa’dah (mwezi wa 11) na Dhul Hijjah (Mwezi wa 12)

Mtume (s.a.w.w) ametuhimiza kufunga katika Mwezi wa Muharram kwa kusema “Funga iliyo bora zaidi baada ya Ramadhani ni funga ya Mwezi Muharram wa Mwenyezi Mungu. Na Swala iliyo bora zaidi ni ile ya Usiku (wa Muharram)” (Sahih Muslim).

Kutajwa huku kwa Muharram kama Mwezi wa Mwenyezi Mungu kwaonesha ni kwa kiasi gani Mwezi huu ni Mtukufu.”

Katika mwezi huu siku ya 10 ya mwezi huu hujulikana kama siku ya Ashura.

Neno Ashura kilugha humaanisha kumi, nani siku muhimu katika historia ya Uislamu kwa sababu ya kuuawa kikatili kwa Mjukuu wa Mtume wetu Mpendwa, Mtume Muhammad (SAWW) SIKU YA ASHURA katika jangwa la Karbala

Waislamu kote ulimwenguni huadhimisha mwezi huu kwa huzuni kubwa kwa kumkumbuka Imam Husain (a.s.), mjukuu wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na Imam (kiongozi wa tatu wa haki aliyeteuliwa na Mtume (s.a.w.w.).

Siku ya mwezi 10 Muharram Imamu Husain (a.s.) aliuliwa kikatili pamoja na wafuasi wake wachache na ndugu zake.