Je, tufanye nini wakati Umma unapokuwa mfu?
Basi yatupasa kufanya nini wakati jamii ikifa? Je, tuiche jamii hii na kwenda kwenye jamii fulani nyingine iliyokufa? Leo (kwa mfano) wanasema kwamba hali katika Pakistan sio nzuri na hivyo wanashauri aina mbili za ufumbuzi; moja ni kuhama, nyingine ni kufanya Taqiya. Maana ya Taqiya kwao wao ni kuacha dini na kujificha ili kwamba usionekane. Kamwe usionekane katika msikiti wowote, Hussainiah, mikusanyiko ya kidini na katika ibada zozote za kidini, kwa vile uko kwenye Taqiya. Hivi ndivyo wanavyoelezea Taqiya kimakosa kama kujificha sehemu fulani, na halikadhalika tafsiri yao ya kugura ni kuiacha jamii mbaya na kwenda kwenye jamii mbaya zaidi. Wanaandika maombi ya Viza ya nchi za Ulaya na kuhamia huko. Wanaiacha jamii hii ya Pakistan ambayo imekufa na kuhamia kwenye jamii mbaya zaidi ya nchi za Ulaya. Huu sio uhamiaji hasa ambamo unahama kutoka jamii moja iliyokufa na kwenda kwenye jamii nyingine iliyokufa, sehemu iliyooza. Kama minyoo katika mzoga wa ng’ombe inahamia kwenda kwenye mzoga wa punda, basi huu hauwezi kuitwa uhamiaji (Hijirat). Wajibu wako wa kwanza sio kukimbia au kujificha, lakini ni kuhuisha jamii hii iliyokufa, kupuliza roho ndani yake na kuihuisha. Lakini kama kwa sababu fulani huwezi kufanya hivyo, basi nenda kwenye sehemu ambayo ina uhai. Ni vigumu sana siku hizi kupata sehemu kama hiyo; kwa hiyo tumeachwa bila chaguo lingine bali kufanya tu juhudi kuihuisha jamii yetu iliyokufa.