Change Language: English

Imam Husein na tabia tukufu za Uislamu

Maamkizi ya Uislamu:

Na kwa kuwa Uislamu unahimiza mwanadamu kuishi katika mazingira ya utamaduni wa amani na salama, kwa ajili hiyo umeweka sharia ya kuanza kuamkia kwa salamu: Asalam alaykum. Imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwamba amesema: "Hakika salamu ni jina miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi lisambazeni baina yanu. Na imepokewa kutoka kwake: "Mtu bakhili zaidi ni bakhili wa salamu. Na imekuja kutoka kwa Abu Ja’far al-Baqir (as) kwamba amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda kutoa salamu. Na mafunzo ya Uislamu yanahamasisha kuanza kutoa salamu ambapo yameifanya kuwa ni sunna. Na imepokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) kwamba amesema: "Kusalimia ni sunna na kujibu salamui ni wajibu. Kwa salamu mwanadamu anatuma ujumbe wa matumaini kwa anayekutana naye na kana kwamba anamwambia: Hutopata kutoka kwangu isipokuwa kheri.

Hivi ndivyoUislamu unavyoandaa utamaduni kwa mwanadamu, ambapo anakuwa ameandaliwa kwaamani na kusaidiana pamojana wenginekatika maisha yake, na utamaduni huu unamsukumakatika kuwafikiria wenginena sio kutia mkazo katika

ubinafsi wake tu. Mkabala wa hilo ni utamaduni wa mabavu, utamaduniunaomfanya mwanadamu awe mbinafsi mwenye kujizingira katika dhati yake tuna raghaba zake na wala hajali mambo ya wengine, utamaduni huuunaandaa mazingiraya ubabe kwa mwanadamukwa sababu hajali wengine na anajali nafsi yake tu, namaslahi yake yanaweza kupelekea kuwafanyia wengine uadui.

Hapa kuna mas'ala muhimu: Utamaduni wa Kiislamu unamlea mwanadamu katika kutozingatia nafsi yake tu, bali inapasa nafsi yake kuwazingatia na wengine pia:

"Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na hisani na kuwapa jamaa na anakataza uchafu na uovu na dhulma. Anawapa mawaidha ili mpate kukumbuka." (Surat Nahli: 90).

Yaani kuwafanyia watu wema, na katika hadithi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema: "Viumbe ni waja wa Mwenyezi Mungu anayependeza zaidi kwake ni mwenye manufaa zaidi kwa waja wake. Mafunzo haya yanamwelekeza mwanadamu kwamba utamu mkubwa anaoustahiki sio tu kutimiza raghaba zake binafsi bali ni ule utamu wa kimaanawiya ambao unapatikana katika kuwahudumia wengine.

Na aliulizwa mmoja wa Maulamaa wema: Kama haitabakia katika umri wako isipokuwa saa moja tu utaitumia wapi? Akasema: “Nitakaa katika mlango wa nyumba yangu nikimsubiria mwenye haja ili nimkidhie haja yake, na hili ndio tunda la mafunzo ya Uislamu.”

Na katika Qur'an Aya nyingi zinamwelekeza mwanadamu kuzingatia haja za wengine bali Qur'an inahimiza kupendelea wengine:

"Na waliofanya maskani na imani yao kabla yao, wanawapenda waliohamia kwao wala hawapati dhiki katika vifua vyao kwa walivyopewa, na wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. " (Surat Hashir: 9).