Distortions of Ashura (21)
Siku ambayo ilishuhudia moja ya mihanga adhimu sana na mikubwa ya wanadamu katika kumbukumbu za kihistoria za kila mwaka. Siku ambayo Imam Hussein (amani iwe juu yake), mjukuu wa pili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) – kupitia kwa Bibi Mtukufu Fatimah – na watu wa familia yake na baadhi ya wafuasi wake wa karibu sana waliuawa kikatili na miili yao kukatwa katwa. Jinai hii ya kikatili sana ilitokea katika jangwa la Karbala nchini Iraqi kwa amri ya Yazid bin Muawiyah, mtawala dhalimu wa ulimwengu wa Waislam kwa wakati huo.
Mbali na mtindo wa maisha ya kishaufu na fahari ya kupindukia, Yazidi bin Muawiyah alifanya kila kilichowezekana katika utawala usio wa Kiislam na usio na maadili ambao haukushuhudia tu uporaji wa hazina ya Ummah bali pia na upuuzaji kamili wa ile misingi yenyewe hasa ya imani za Kiislam na Qur’ani Tukufu.
Taswira tukufu ya Imam Husein (kama mrejelewa pekee kutoka kwenye nyumba tukufu ya bwana Mtume (s) wa zama hizo) pamoja na wafuasi wake ulikuwa kikwazo kwa Yazid bin Muawiyah na alimuamrisha Imam kutoa kiapo cha utii kwake. Majibu ya kihistoria ya Imam Husein (a.s.) yatarindima daima katika historia ya binadamu kwa vile huweka bayana nguvu za uovu na wema, haki na batili, uadilifu na dhulma yote ni ukweli dhahiri wa kila zama. Na kupitia kweli hizi Mwenyezi Mungu huwajaribu binadamu Wake kwazo.
“Kifo cha heshima ni bora kwangu kuliko maisha ya aibu na fedheha. Mtu wa mfano wangu mimi hawezi kamwe kutoa kiapo cha utii kwa watu mfano wa Yaziid.”
Hili ndio lilikuwa jibu la Imam Husein (amani iwe juu yake) kwa wajumbe wa Yazid bin Muawiyah.
Imam Husein – mfano halisi hasa wa kanuni za msingi wa ki-Tawhiid ya Kiislam, wakati alipokabiliwa aliwatamkia maadui zake ambao walikiri kuwa Waislam chini ya bendera ya Yazid bin Muawiyah kwa kusema:
“Mimi sikutoka kama dhalimu; wala kama mtu anayetaka kusababisha uharibifu; na wala sikutoka mimi bali kwa ajili ya kutengeneza ummah wa Babu yangu kwa “kuamrisha mema” (Amr bil-Maaruf) na kukataza maovu (Nahi-anil-Munkar)’”
Muhanga huu wa sifa kubwa daima kwa ajili ya (haki na uadilifu) wa Imam Husein na familia yake ya karibu kabisa, ikiwa ni pamoja na mtoto wa umri wa miezi sita, na baadhi ya wafuasi wake – wazee wa umri mkubwa kuweza kuwa ma-babu – ulitingisha ulimwengu wa Kiislam kutoka kwenye minyororo ya uharibifu wa maadili na unyofu. Sababu iliyoko nyuma ya kupoteza thamani kusiko kwa Kiislamu (iliyokusanywa kwa kipindi cha takriban miongo mitano baada ya kifo cha Mtukufu Mtume) chini ya watawala madhalimu wa kujibandika wenyewe wa ufalme wa ki-Bani Ummayyah daima ukawa umefichuliwa. Muhanga huo ukiwa umegeuka kuwa mnara wa kudumu wa msukumo wa kutia moyo kwa waumini na wanyonge wanaokandamizwa.
Karbala, mazingira yaliyomkabili Imam Husein (a.s) na athari zilizotolewa kwenye mazingira hayo zinawasilisha mfano wa kufuatwa na wapenda haki, ukweli na heshima wote. Karbala imewazindua mamilioni ya watu kurekebisha, sio tu nafsi zao wenyewe bali pia na jamii zao, kuondosha dhulma, unafiki, ujinga na undumilakuwili. Muhanga wa Imam Husein (a.s) na familia yake tukufu unatuachia sisi dhima ya kuwa watu mashughuli kwenye jamii yetu ili kufanya kazi kuelekea kwenye maadili matukufu ya kawaida kama vile ukweli, haki, uadilifu na usawa.
Hakuna jamii inayoweza kuwa imetulia au ikastawi bila ya kanuni hizi ambazo zimekuwa msisitizo wa msingi wa Qur’ani tukufu, Bibilia, Tawrati na vitabu vyote vya mbinguni. Jamii inapaswa kuungana pamoja na kushirikiana katika kufanikisha maadili haya matukufu ambayo yanashambuliwa na kuondolewa na utamaduni wa kimagharibi na vyombo vyao vya habari. Utamaduni na vyombo vya habari vya magharibi vinaeneza uchochezi, mahusiano yasiyo na ulinzi kati ya wanaume na wanawake, uasherati, ufitini, uyakinifu, ubinafsi, choyo na udanganyifu. Mapambano ya Imam Husein (a.s) yalikuwa ni muhanga mkubwa na muhimu dhidi ya maovu haya na ule mfumo unaoyaunga mkono na kuyatia chachu. Sisi vilevile leo hii tunapaswa kushutumu mifumo na athari hizi ili kuweza kuwa huru na watu wa Mungu.