Change Language: English

SIKU YA ASHURAA

“Sema: kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa walionikurubia.”(42:23) Masahaba waliuliza; “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu !
Ni nani hao jamaa zako wa karibu ambao mapenzi kwao imefanywa wajibu juu yetu?”
Bwana Mtume (s.a.w.w.) alijibu; hao ni, “Ali, Fatima, Hassan na Hussein.” (as)

Taz: Durrul Manthur J. 6, uk. 7, Musnad Ahmad J. 2, uk. 669/1141, Al Kashshaf J. 4, uk.
219 Zamakhshari na Fakhrudin-Razi ndani ya tafsiri zao za Kurani wanasimuliya hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) inayosema; “Anayekufa akiwapenda watu wa Nyumba ya Bwana Mtume, (s.a.w.w.) amekufa kifo cha shahid; madhambi yake yatasamehewa na imani yake itahesabiwa iliyokamilika.”Wanaendelea kusimulia hadithi nyingine ya
Mtume (s.a.w.w.) inayosema; “Anayekufa akiwachukia watu wa Nyumba ya Bwana
Mtume (s.a.w.w.) amekufa kifo cha kijahiliya na hatoweza hata kunusa harufu ya
peponi.”

Aya nyengine inasema; “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na kukutakaseni sana sana.”Iliposhuka aya hii, Mtume alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein (as) akawafunika guo (kisaa), kisha akasema, “Ee Mola! Hawa ni watu wa nyumba yangu (Ahlul-bait), basi waondolee uchafu na uwatakase sana sana.” Mama Ummu Salama (mkewe Mtume) alipotaka kuingia pamoja nao katika hilo guo, Mtume akamzuia. Mpaka hapa tushaona utukufu usio mfano wa watu wa nyumba ya Bwana Mtume.(s.a.w.w.) Ibne Abbas anasema robo tatu ya kurani imewashukia wao (Nyumba ya Bwana Mtume). Subhana-llah.

Taz: Tafsirul Tabari J. 33, uk. 5-7, Al-Mustadrak J. 2, uk. 416, Sahih Muslim J. 4,
uk. 127

Imam Husein (as) alipokuwa anaondoka Madina kabla ya kifo chake, alikwenda kaburini
kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) kumuaga, akapata usingizi, akamwona Bwana Mtume (s.a.w.w.) anamwambia, Mimi (Mtume), Babayako (Ali), Mama yako (Fatima) na Kaka yako (Hasan) tunakusubiri kwa hamu, karibu utajiunga nasi.

Mwezi pili Muharram, Imam Hussein alifika Karbala na mwezi saba Muharam jeshi la
Yazid lilimfungia maji wa mto Furat Ashuraa, siku ya huzuni na msiba mkubwa kwa
Uislamu, Yazid bin Muawiya bin Abu-Sufyan alimuua mjukuu wa Bwana Mtume, Imam
Hussein na watu wake sabini na mbili akiwemo mtoto wa miezi sita. Haya ndio malipo
tunayomlipa Bwana Mtume kwa kumuuliya Hussein? Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanatuusia tuwapende watu wa Nyumba
ya Mtume, lakini Yazid na majeshi yake yanawaua. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)
alimlilia Husein,(as) kama anavyotusimulia mke wa Mtume, Ummu Salama, alimwona
Mtume katika ndoto analia, ndevu na nywele zake zimejaa vumbi, anamwambia mwanangu Husein (as) ameuawa Karbala. Alipozaliwa Husein, Malaika Jibrail alimwarifu Mtume, (s.a.w.w.) kwamba umma wako utamuua. Mtume alilia sana. Mbingu na ardhi zilimlilia Hussein. (as)

Taz: Tabari

Inashangaza kuona Ahlul-Bait waliotoa roho zao, mali zao, kuutetea Uislamu wakati wa uhai wa Bwana Mtume, (s.a.w.w.) wakaonekana maadui baada ya kifo chake. (Mtume)
Abu-Sufyan na ukoo wa banu ummaya, maadui wakubwa wa Bwana Mtume na Uislamu, wakawa watu wema baada ya kifo chake.

“Ewe nafsi yenye kutua! Rudi kwa Mola wako hali ya kuridhia (na) mwenye kuridhiwa.
Basi ingia katika waja wangu (wema). Na ingia katika pepo yangu.” Surat-Fajr
:27-30.