Uislamu Na Majeshi Ya Kuzuia Mapambano
Sheria, matendo na desturi za Uislamu, kwa ufupi, mfumo wake wa kijamii, ulianzisha wakati wa uhai wa Mtume. Kwa kusababisha mabadiliko haya makubwa, ilimbidi avumilie machungu mazito sana mateso na matatizo makubwa kwake yeye mwenyewe na akakabiliana na upinzani mkali kabisa kutoka kwa wale ambao nafasi yao ya utawala ilitishiwa na Uislamu.
Miongoni mwa mambo mengine, kwa mfano, ulipiga marufuku utozaji na ulipaji wa riba, ukaondoa chanzo chenye manufaa cha mapato kwa wale ambao waliutumia mpango huu. Uislamu pia ulifundisha kwamba utukufu miongoni mwa watu, sana ulitegemea juu ya ubora wa tabia (mwenendo) wa utekelezaji kamilifu kabisa wa wajibu wake mtu.
Hili lilikuwa tishio la hatari sana kwa wale ambao hadhi zao katika jamii zilitegemea kabisa juu ya mali, utajiri na rasilimali za kimaada zilizo sawa na hizo. Kinyume cha hayo, Uislamu uliendeleza kuwepo matumaini kwa mtu masikini sana kupata heshima na utukufu kama atakuwa ametimiza yale yaliyotakiwa kwake katika utekelezaji wa wajibu wake na uchamungu.
Bani Umayyah chini ya uongozi wa Abu Sufyan, wakichochewa na wingi wa uadui na wivu wa zamani na wa karibuni, waliuongoza upinzani kwa Mtume. Alirushiwa mawe. Malundo ya uchafu yalitupwa juu yake na usumbufu mwingi usio na mwisho, mateso na udhalilishaji vilitumiwa dhidi yake. Maisha yake yalitishwa na ami yake, Abu Talib, alimwondoa na kumpeleka kwenye sehemu ya usalama ya ngome yake ya mlimani ambako huko waliipitisha (walikaa) miaka mitatu kwa kujitenga kabisa. Maquraishi walikataa kabisa maingiliano (ushirikiano) ya kijamii na Bani Hashim.
Ndani ya mwaka mmoja wa ufungaji wa sura hii ya msuso wa kijamii, ami yake Mtume, Abu Talib, na mkewe kipenzi, khadija, walifariki dunia na upinzani kwa Mtume ulibuni njama ya kumuua (Mtume). Alitorokea Madina, akimwacha Ali, binamu yake, akiwa amelala fofofo kitandani mwake.
Hata huko Madina Mtume na wafuasi wake hawakupata nafuu yoyote ile kutokana na vitendo vibaya visivyo vya huruma vya maadui zake ambao waliishambulia Madina zaidi ya mara moja, hata kumlazimisha Mtume kupingana nao.
Vita vya kwanza vya Uislamu, vilipiganwa Badr ambamo Waislam 314 tu,1waliokuwa na farasi watatu tu,2 kwa mafanikio makubwa waliyashinda majeshi yaliyokuwa bora na imara ya Bani Ummayah. Hamza bin Abdul Muttalib, Ubaydah bin Harith na Ali bin Abi Talib walikuwa miongoni mwa mashujaa maarufu wa Bani Hashim.
Ali alifanya mambo makubwa ya ajabu ya ushujaa kiasi kwamba maadui walivunjika moyo. Hasara ya kuhuzunisha kwa Bani Hashim ilikuwa kwamba Ubayda aliuawa. Upande wa Bani Umayyah ulipata hasara nyingi: mtoto wa Abu Sufyan, Hanzal, aliuawa na Ali, ambaye alimchukua mateka mwingine katika watoto wake, (aliyeitwa) Amr. 3
Hind, mke wa Abu Sufyan aliomboleza vifo vya baba yake, Utba; ami yake, Shayba; na nduguye, al-Walid 4. Misiba hii ilimzidi nguvu Abu Sufyan kiasi kwamba aliweka nadhiri ya kutokuoga mpaka awe ameon- goza mashambulizi dhidi ya Mtume.
Vita nyingine muhimu kati ya Mtume na makafiri vilipiganwa katika mwaka wa 3 A.H. kule Uhud.5 Abu Sufyan alikuwa amekusanya jeshi la askari 3,000 wakati Mtume alikuwa na wanajeshi wapatao 700 tu,6 na farasi wawili. Idadi kubwa ya wanawake ilifuatana na Abu Sufyan kulitia ari na moyo jeshi lake kwa muziki wao wa kijeshi na nyimbo. Hapa pia, Waislam walishinda kupitia ushika upanga mahiri na bora wa Ali bin Abi Talib.
Hamza, ami yake Mtume aliuawa katika vita hivi, na Hind mke wa Abu Sufyan katika kudharau mwenendo wote mwema wa kibinadamu alilichomoa ini lake na akajaribu kulila. 7 Alijipamba kwa kuvaa masikio na viungo vingine vya miili ya wale waliouawa katika vita. Matendo hayo ya kinyama huonyesha kusisitiza kuwepo kwa chuki ya muda mrefu ambayo Bani Umayyah walikuwa nayo dhidi ya Hashim kwa ujumla na hususan kwa Mtume mwenyewe.
Maquraishi walifanya jaribio la mwisho katika mwaka wa 5 A.H. kuupiga Uislamu na kuumaliza. Walifanikiwa kuwapata Mayahudi kwenye kusudio lao na wakaibuka na jeshi lenye askari 10,000 kwa ajili ya “vita ya Makundi” dhidi ya waislam ambao idadi yao ilikuwa ya watu 3,000.
Maadui hawa wa Uislamu kwa mara nyingine tena walishindwa na shujaa wao Amr bin Abd-Wudd alianguka chini kwa upanga wa Ali (aliuawa).
Na hapo Abu Sufyan aliondoka kwenda Makka akiwa amevunjika moyo na tamaa ya kupigana tena na Mtume ikawa imevunjwa kabisa moyoni (mwake).
Alipoona kwamba Maquraishi hawakudhihirisha ishara za uvamizi kwa kipindi kirefu kidogo, Mtume aliongoza baadhi ya Waislam kwenda Makka kufanya Umra au Hijja ndogo, pamoja na ngamia wa kuchinja kuwatoa kafara. Alipogundua kwamba Khalid bin al-Walid alikuwa anajiandaa kumzuia, Mtume aliiacha njia aliyokuwa anaifuata.
Tendo hili la Mtume la kipatanishi lilipelekea kutiwa sahihi kwa mkataba wa amani kati yake na Maquraishi. Mkataba huo ulipiga marufuku vita kati ya makundi hayo kwa kipindi cha miaka kumi, na ukaacha wazi kwa wengine kujiunga na upande wowote waupendao. Iliamuliwa kwamba Waislam wangerudi bila ya kutekeleza ibada hiyo ya Hijja na warudi tena Makka katika mwaka ufuatao na kuikamilisha hija hiyo ndogo ya Umra ndani ya muda wa siku tatu tu na kisha wautoke mji.
Pia (mkataba) huo uliandaa kwamba mtu yeyote yule atakayetorokea kwenye kundi la Muhammad bila ya ruhusa ya mlezi wake lazima arudishwe kwa mlezi wake, lakini kama Quraishi akitoka kwenye ufuasi wa Muhammad huyo asirudishwe. Baadhi ya masharti haya yalikuwa kwa wazi kabisa yasiyo na manufaa kwa Waislamu na baadhi yao walifikiria kuwa ni dalili ya unyonge kutia saini mkataba kama huo. Kwa kweli misingi ya imani ya baadhi ya Waislam ilitingishwa na mkataba wa Hudaibiyyah, kama unavyoitwa.
Mtume aliyakubali masharti yasiyolingana ya mkataba huu ili kukwepa kushutumiwa kwa uchokozi. Aliyachunga masharti ya mkataba kwa maandishi na mazingatio. Mtume alirudi Makka mwaka uliofuata na akatekeleza hijja ndogo ya Umra kama ilivyoelezwa katika mkataba.
Makabila ya Khuzaa na Bakr yalikuwa na hisia za uadui yenyewe kwa yenyewe zilizojengeka kwa muda mrefu, kabila la Khuzaa lilikuwa lenyewe limejishirikisha kwa Mtume, na kabila la Bakr lilijiunga na makafiri.
Mkataba wa amani, kama tulivyokwishaona ulitoa haki ya kukomesha uhasama kati ya makundi haya kwa kipindi ya miaka kumi, na kwa maana hii, hili pia lilitumika kwa makundi yaliyoungana na watiaji sahihi wakuu wa mikataba huo. Kwa hiyo watu wa kabila la Khuzaa waliweka chini silaha zao na wakashtukizwa kwa ghafla na kabila la Bakr ambao kwa siri wakisaidiwa na Maquraishi, waliwaua watu wengi wao wakati wakiwa katika sala zao.
Maelezo ya mauaji haya makubwa yalisimuliwa kwa huzuni kubwa kwa Mtume na msaada wake ulitafutwa kwa kusihiwa sana kiasi kwamba mara moja alikwenda Makka kuwasaidia watu wa kabila la Khuzaa, akiwa amekasirishwa sana na uvunjwaji wa masharti ya mkataba na kwa tabia ya kikatili na ya kufehedhesha ya Maquraishi.
Makafiri walikuwa katika mtawanyiko kabisa na alipogundua hakuna njia nyingine zozote zile za kusalimisha maisha yake, Abu Sufyan aliingia katika Uislam.8 Mtume wa Uislamu alitoa msamaha siyo kwake tu (Abu Sufyan) bali aliufikisha kwa wale ambao walipata hifadhi ndani ya nyumba yake.
Kisha akawaacha huru watu wote wa Makka. Baada ya haya, hata Hind mke wa Abu Sufyan aliukubali na kuingia katika Uislam kama kwa hakika walivyofanya watu wote maarufu wa kabila la Maquraishi.
Kukubali Uislamu kwa Bani Umayyah na wapinzani wengine wa Uislamu hakukulazimu kuleta badiliko katika hisia zao halisi kuhusu Mtume.