Change Language: English

MWANGAZA KUTOKA KATIKA MAISHA YA IMAM HUSAIN (AS)

Tarehe tano ya mwezi wa Shabani katika mwaka wa nne Hijiriailichomozanuru ya Husain (as) katika nyumba tukufu ya Ali (as).

Kupewa kwake jina:

Babu yake, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alimpa jina Husain (as) kama alivyompa jina kaka yake Hasan (as) ambaye alizaliwa kabla yake, na hayo ni majina mawili ambayo hayakuwa yakijulikana bali yalifunuliwa kwa Nabii (saww) kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Imepokewa kutoka kwa Imran bin Sulaiman kuwa alisema: "Hasan na Husain ni katika majina ya watu wa peponi hayakuwepo wakati wa ujahiliya.

Familia yake.

Husain (as) anatokana na ukoo mtukufu na familia tukufu katika historia ya binadamu, babu yake kwa upande wa mama yake ni Mtukufu Mtume (saww) na baba yake ni Kiongozi wa Waumini Ali bin Abi Twalib (as), na mama yake ni Bibi mbora wa wanawake wote wa ulimwengu Fatma Zahra binti ya Mtukufu Mtume.

Katika Qur'ani Tukufu:

Husain (as) ni mtu wa tano katika watu wa kishamiya ambao kwao iliteremka aya ya kuwatakasa:

4$yJ¯RÎ)߉ƒÌãƒª!$#|=Ïdõ‹ã‹Ï9ãNà6Ztã}§ô_Íh9$#Ÿ@÷dr&ÏMøt7ø9$#ö/ä.tÎdgsÜãƒur#ZŽÎgôÜs?ÇÌÌÈ

"Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa."

Na maelezo yafuatayo yamekuja katika tafsiri ya Ruhul-Maaniy ya al-Alusiy al-Baghidadiy kuhusu aya hii tukufu:

“Amepokea Tirmidhiy na al-Hakim na wamesema ni riwaya sahihi, na Ibnu Jarir, Ibnu Mundhir, Ibnu Marduwayhi na Bayhaqiy katika Sunan yake kutoka katika njia ya Ummu Salama (r.a), amesema: ‘Katika nyumba yangu iliteremka ‘Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.’ Na ndani ya nyumba alikuwemo Fatma, Ali, Hasan na Husain, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) akawafunika kwa kishamiya kisha akasema: Hawa ni watu wa nyumba yangu basi waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.’”

Na imepokewa kutoka kwa jamaa kutoka kwa Umar bin Abi Salama mtoto wa kulea wa Mtukufu Nabii (saww), amesema: Ummu Salama alisema: ‘Je na mimi niko pamoja nao?’ Akasema (saww): ‘Wewe uko mahala pako, na hakika wewe uko katika kheri.’ Na habari za Mtume (saww) kumwingiza Ali, Fatma na watoto wao (r.a) ndani ya guo na kutomwingiza Ummu Salama ni nyingi na hazihesabiki, nazo ni zenye kuainisha ni akina nani watu wa nyumba ya Mtume (saww) kwa maana yoyote ile ya nyumba,

na makusudio ni wale waliofunikwa kwa guo, na wala hawaingii humo wake zake.”

Na Husain (as) ni katika jamaa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ambao Mwenyezi Mungu amefaradhisha kwa Waislamu wajibu wa kuwapenda katika kauli yake (swt):

@è%Hwö/ä3è=t«ó™r&Ïmø‹n=tã#·ô_r&žwÎ)no¨ŠuqyJø9$#’Îû4’n1öà)ø9$#3ÇËÌÈ

"Sema: kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu."

al-Hafidh as-Suyutiy as-Shafi'iy amesema: “Amepokea Ibnu Mundhir, Ibnu Abi Haatim na Ibnu Marduwayhi katika tafsiri zao, na Tabaraniy katika Muujamul-Kabiyr kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa amesema: ‘Iliposhuka aya hii "Sema: kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika ndugu." Walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni nani ndugu zako hawa ambao imekuwa ni wajibu kwetu kuwapenda? Akasema (saww): Ni Ali, Fatma na watoto wao.’”

Manukato ya Mtume (saww):

Imepokewa kwa tawatur kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) hadith nyingi zinazoeleza wajibu wa kumpenda sana mjukuu wake Husain (as) na ndugu yake Hasan (as), na humo anabainisha nafasi yao na fadhila zao katika masikio ya masahaba wake kama vile kauli yake (saww):

هما ريحانتاي من الدنيا

“Wao ni manukato yangu katika dunia.”

Na kutoka kwa Ya'aliy bin Murrah amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww):

حسين مني وأنا من حسينأحب الله من أحب حسينا، حسين سبط من الأسباط

“Husain anatokana na mimi na mimi ninatokana na Husain, Mwenyezi Mungu anampenda mwenye kumpenda Husain, Husain ni mjukuu kati ya wa wajukuu."