Change Language: English

Mkesha Wa Mwezi 10 Muharam

Lengo kuu la msingi alilolitamani sana Husein ambalo kwalo aliomba kusimamishwa mapigano kwa muda, lilikuwa kumwezesha yeye na sahaba zake kuutumia usiku huo wa mwisho wa uhai wao katika Sala na du’a kwa Mwenyezi Mungu, kusoma Qur’ani Tukufu na kumwomba Allah Mwenye Nguvu zote kwa ajili ya rehema Zake. Moja ya malengo mengine muhimu ya kutaka uakhirisho huu mfupi ni kwamba alipenda kuwapa marafiki na maadui pia, fursa nyingine ya kuchunguza usawa wa msimamo waliochukua katika vita hii, kuchagua, bila hofu au upendeleo, njia iliyo bora zaidi, kwa vile sasa mauti yanaonekana kuwa dhahiri kwa marafiki zake, na sio kwa uhakika kabisa kwa wengi wa maadui zake. Kuingia kwa jioni ya siku ya 9 ya Muharam Husein, aliwaita ndugu na marafiki zake, na baada ya kuwatolea heshima za juu kwa uaminifu wao kwake na sifa nyingine zilizo bora, alisema: “Vita ni hakika mno vitapiganwa kesho. Ninavifungua viapo vyenu vyote vya utii kwangu na ninakupeni ruhusa kamili kuondoka na kwenda popote pale ambapo mngependa kwenda. Litumieni giza la usiku na muondoke. Kila mmoja wenu anaweza pia kuushika mkono wa mmoja wa ndugu zangu na kuon- doka naye pia. Kwani maadui wana kiu ya damu yangu tu, na mara watakapokuwa wameshaniua hawatamtafuta mwingine yeyote yule.1 Abbas bin Ali, ndugu yake Husein alisimama na akasema, “Kwa nini tufanye kama ilivyopendekezwa? Kuishi baada yako wewe hakuna faida. Hapana, Mwenyezi Mungu atuweke mbali na siku nyeusi kama hiyo!” Hisia za namna hii zilielezwa pia na kizazi cha Aqil. Kisha Muslim bin Awsaja alisimama, na alisema: “Hatuna uwezo wa kukutelekeza wewe. Nitapigana kwa mkuki…kwa upanga wangu na kama nikikosehswa silaha, nitawashambulia kwa kuwatupia mawe mpaka niwe nimejitoa mhanga maisha yangu miguuni mwako.” Saidi bin Abdillah al-Hanafi alisema, “…Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba kama nikitambua kwamba nitauawa kwa upanga, na nikarudishwa tena kuwa hai, na kisha ningeunguzwa nikiwa hai, na majivu yangu yakatawanywa hewani na kwamba ningetendewa vivyo hivyo mara sabini, sitakuwacha mpaka wakati wa mwisho nifie miguuni mwako.” Zuhair bin Qayn alisema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu, ni hamu yangu ya dhati kuuawa kwa upanga, nifufuliwe na halafu tena niuawe. Hivi inaweza kurudiwa mara elfu moja kama msiba unaokaribia kutokea unaweza kuepushwa kutokana na kukupata wewe na watu hawa mashujaa wa familia yako.” Hisia kama hizi za uaminifu thabiti na utiifu kwa Husein zilielezwa na masahaba wengine wa Husein. Husein hakufanya jitihada zozote kuwaweka watu pamoja naye kwa kuamsha hisia zao au kuyalea matumaini ya uwongo au hamu kubwa ya kupata kitu. Badala yake aliwataka wafuasi wake waende kwenye usalama kama nafasi yoyote ile ya kufanya hivyo itapatikana. Siku ya mwezi 10 Muharram, ilitangaa kwamba Amr, mtoto wa Bishr bin Amr al-Hadramin, alikuwa amekamatwa katika mipaka ya Rayy. Bishr alisema kwamba alim- toa mtoto wake na yeye mwenyewe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwamba kama ataishi asingependa kuona mtoto wake anakuwa kizuizini. Husein aliyasikia haya na akamwita Bishr kwake akamwambia kwamba amemfungulia na kumwacha huru kutokana na kiapo chake cha utii na anaweza kwenda kumtoa mtoto wake kizuizini. Bishr alijibu: “Wanyama wakali walao nyama wanimeze nikiwa ningali hai, kama ningekuwa mimi ni mwenye kukuacha wewe. Mambo haya yatawezekana vipi?”. Kisha Husein alimtaka ampeleke mmoja wa wanawe mwingine, aitwaye Muhammad, aende kwa nduguye na akampatia nguo zenye thamani kiasi cha dirham 1000.” Kama ilivyokwishatajwa, lengo la Husein katika kuomba kusitishwa vita kwa muda wa usiku mmoja lingewezekana vile vile kukusudiwa kuwapa adui zake muda wa kufikiria sifa stahilifu za dhuria wahusikao katika vita hivi na kupata uamuzi wao wa mwisho kuwahusu hao. Kukimbia kwa Hur na wanajeshi wachache wa jeshi la Umar bin Sa’d kwenda kujiunga na jeshi la Husein katika siku ya 10 ya Muharam huonyesha mafanikio aliyoyapata Husein katika kuudhihirisha ukweli wa njia yake kwa wale ambao walikuwa tayari kumsikiliza na kufikiria kwa uhuru. Husein na jamaa zake aliutumia usiku huu katika maombi na Sala kwa Mwenyezi Mungu kumwomba na kumsihi sana, waliutumia pia katika kusoma Qur’an na kufanya matendo mengine yafananayo na haya, huku mrindimo wa sauti zao ukiuvunja ukimya wa usiku kama nyuki wavumao. Hatua za kuhakikisha usalama zaidi kwa taratibu zilizokuwepo wakati wa vita zilichukuliwa. Mahema yalikitwa karibu zaidi kila moja na lingine na kamba za kila hema ziliimarishwa kwa kuzifunga pamoja na zile za mahe- ma yaliyo karibu. Mwinamo wa nyuma wa mahema ulifanywa kuwa na kina zaidi ili kufanya handaki. Kuni zilipangwa ndani yake ili kwamba wakati lilipowashwa moto, kusingekuwa na shambulizi la adui ambalo lingekuwa rahisi kuongozwa dhidi ya mahema kutoka upande wa nyuma.