Change Language: English

IMAM HUSEIN NA SIKU YA ASHURA

Mwezi wa Muharram ndio mwezi wa kwanza katika kalenda ya Kiislam. Tarehe 10 ya Muharram mwaka huu itaangukia tarehe 6 Desemba, 2011 kulingana na mwaka 1433 wa kalenda ya Kiislam. Siku hii inajulikana kwa Waislam kama Siku ya Ashura.

Siku ambayo ilishuhudia moja ya mihanga adhimu sana na mikubwa ya wanadamu katika kumbukumbu za kihistoria za kila mwaka. Siku ambayo Imam Hussein (amani juu yake), mjukuu wa pili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) – kupitia kwa Bibi Mtukufu Fatimah – na watu wa familia yake na baadhi ya wafuasi wake wa karibu sana waliuawa kikatili na miili yao kukatwa katwa. Jinai hii ya kikatili sana ilitokea katika mawanda ya Karbala nchini Iraqi kwa amri ya Yazid bin Muawiyah, mtawala dhalimu wa ulimwengu wa Waislam kwa wakati huo.

Mbali na mtindo wa maisha wa kishaufu na fahari ya kupindukia, Yazidi bin Muawiyah alifanya kila kilichowezekana katika utawala usio wa Kiislam na usio na maadili ambao haukushuhudia tu uporaji wa hazina ya Ummah bali pia na upuuzaji kamili wa ile misingi yenyewe hasa ya imani za Kiislam na Qur’ani Tukufu.

Uwepo wa sura Tukufu ya Imam Husein pamoja na wafuasi wake ulikuwa usiokubalika kwa Yazid bin Muaiyah na aliamuamuru Imam kutoa kiapo cha utii kwake. Majibu ya kihistoria ya Imam Husein (a.s.) yatarindima daima katika historia ya binadamu kwa vile nguvu za uovu na wema, haki na batili, uadilifu na dhulma yote ni ukweli dhahiri wa kila zama. Na kupitia kweli hizi Mwenyezi Mungu huwajaribu binadamu Wake kwazo.

“Mtu wa mfano wangu mimi hawezi kamwe kutoa kiapo cha
utii kwa watu mfano wa Yaziid.”
Hilindio lilikuwa jibu la
Imam Husein (Amani juu yake) kwa wajumbe wa Yazid bin Muawiyah.

Imam Husein – ile mfano halisi hasa wa kanuni za
msingi wa ki-Tawhiid ya Kiislam, wakati alipokabiliwa aliwatamkia maadui zake
ambao walikiri kuwa Waislam chini ya bendera ya Yazid bin Muawiyah kwa kusema: “Mimi sikutoka kama dhalim; wala kama mtu anayetaka kusababisha uharibifu; na wala
sikutoka mimi bali kwa ajili ya kutengeneza ummah wa Babu yangu kwa “kuamrisha
mema” (Amr bil-Maaruf) na kukataza mabaya (Nahi-anil-Munkar)’”

Muhanga huu wa sifa kubwa daima kwa ajili ya (haki na uadilifu) wa Imam Husein na familia yake ya karibu kabisa, ikiwa ni pamoja na mtoto wa umri wa miezi sita, na baadhi ya wafuasi wake – wazee wa umri mkubwa kuweza kuwa ma-babu – ulitingisha ulimwengu wa Kiislam kutoka kwenye minyororo ya uharibifu wa maadili na unyofu. Sababu iliyoko nyuma ya kutu ya Kiislam (iliyokusanywa kwa kipindi cha takriban miongo mitano baada ya kifo cha Mtukufu Mtume) chini ya watawala madhalimu wa kujibandika wenyewe wa ufalme wa ki-Bani Ummayyah daima ukawa umefichuliwa. Muhanga huo ukiwa umegeuka kuwa mnara wa kudumu wa msukumo wa kutia moyo kwa waumini na wanyonge wanaoonewa.

Mwezi wa Muharram (mavazi meusi yakiwa ndio ishara ya huzuni), huwa unaadhimishwa kote katika ulimwengu wa Kiislam sio tu kwa hutoba zenye maana kabisa (za kuukumbusha ulimwengu) juu ya usaliti ambao nyumba ya Mtukufu Mtume iliupitia (katika mapambano yao kwa ajili ya haki na uadilifu baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume wa Uislam); lakini pia kwa kushutumu na kulaani aina zote za dhulma, uonevu na batili.

Waislam wakati wa hotuba hizi wanakumbushwa juu ya wajibu wao mtukufu kwa Mwenyezi Mungu, Uislam na ubinadamu kwa jumla na uhakika wa Siku ya Kiyama na matokeo ya mwisho ya matendo yake mtu.

Tembelea Tovuti yetu kwa maelezo zaidi juu ya Uislamu:
www.al-islam.org/sw / www.issuu.com/alitrah /http://afroshia.blogspot.com

Kwa maelezo zaidi juu ya Imam Husain (Amani juu yake)
unaweza kuwasiliana nasi kwa barua pepe: alitrah@yahoo.com or bilaltz@africafederation.org