Change Language: English

​ Husain (as) anapinga Kiapo cha utii:

Yazid akamwandikia gavana wa Bani Umayya katika mji wa Madina, Walid bin Utba bin Abi Sufian akimtaka kuchukua kiapo cha utii kwa nguvu kutoka kwa masahaba wakubwa na miongoni mwao ni Imam Husain (as).

Usiku wa manane Husain (as) aliitwa kwenye kikao na Walid na akatakiwa kutoa kiapo cha utii kwa Yazid, Imam akajibu: “Hakika aliye mfano wangu hatoi kiapo cha utii kwa siri wala hakichukuliwi kutoka kwangu kwa siri, utakapotoka mbele ya watu na kuwataka watoe kiapo cha utii, basi hapo ndipoutakaponiita na mimi pamoja nao na jambo letu litakuwa moja.” Walid akakubali maneno ya Imam Husain (as) lakini Mar'wan bin al-Hakam aliyekuwa amekaa pembeni mwa Walid akakataa aliyoyasema Husain (as) na akamtaka Walid amlazimishe Husain (as) atoe kiapo cha utii haraka.

Na ili kujibu kitisho hiki, Imam Husain (as) alitangaza msimamo wake wa kupinga kutoa kiapo cha utii kwa Yazid kwa kusema:

Husain anaondoka Madina:

Imam Husain (as) aliondoka mji mtukufu wa Madina tarehe 28 Rajab mwaka 60 Hijiria kuelekea mji mtukufu wa Makka, hiyo ni baada ya kumwachia ndugu yake Muhammad bin al-Hanafiya wasia aliobainisha humo lengo la kutoka kwake na harakati zake, ambapo imekuja humo:

Aliwasili Makka tarehe 3 Shaaban na akaanza kutangaza msimamo wake huko na kueleza rai yake kuhusu utawala wa Bani Umayya katika mkusanyiko wa Waislamu ambao waliwasili katika Nyumba tukufu kwa ajili ya Hija na Umra. Kama ambavyo Imam (as) pia alituma barua zake kwa wakuu wa Iraki huko Kufah na Basra akiwaeleza msimamo wake wa kupinga utawala wa Yazid na akiwataka wamuunge mkono na kumsaidia.

Mwitikio wa Kufah:

Mazingira ya mji wa Kufah yalikuwa yako tayari kwa mapinduzi dhidi ya utawala wa Bani Umayya, kwa hiyo watu wa Kufah walikubaliana na msimamo wa Imam Husain (as), na wakamtumia wajumbe na wakaandika maelfu ya barua wakitangaza kiapo chao cha utii kwake na utayari wao wa kumuunga mkono. Wanahistoria wanasema: Zilikusanyika kwake kwa nyakati tofauti barua elfu kumi na mbili na ikamfikia orodha ya majina 140,000 wakieleza dhamira na utayari wao katika kumsaidia na kumuunga mkono pindi atakapowasili Kufah, kama ambavyo zilipokewa kwake kwa siku moja barua mia sita. Ndipo Imam Husain (as) akamtuma kwao mtoto wa ami yake Muslim bin Aqiyl ili akaone uhalisia wa mazingira ya Kufah na achukue kiapo cha utii kutoka kwao kwa niaba ya Imam na aandae mambo kwa ajili ya ujio wa Imam.

Muslim aliondoka Makka usiku wa nusu ya mwezi wa Ramadhan na alifika Kufah tarehe 5 ya mwezi wa Shawwal, ambapo alipokelewa na watu wake kwa furaha na bashasha, na watu wakajitokeza kumpa kiapo cha utii kama mwakilishi na balozi wa

Imam Husain (as), akamwandikia Imam akimpa habari njema jinsi watu walivyomkubali na kumpa kiapo cha utii na akimhimiza kuharakisha kwenda Kufah.

Lakini Mtawala wa Bani Umayya ambaye aliogopeshwa na uasi wa Kufah dhidi ya utawala wake aliharakisha kumuuzulu gavana wa Kufah Nu'uman bin Bishir kwa udhaifu wake katika kukabiliana na uasi, na Yazid bin Muawiya akamteua badala yake Ubaidullah bin Ziyad ambaye ni maarufu kwa ukatili wake na ubabe wake. Baada ya Ibn Ziyad kushika hatamu za ugavana wa Kufah akapanga kwa hila na ulaghai na akatumia mbinu kali za ukandamizaji na vitisho ili kumaliza uasi wa wafuasi wa Imam Husain (as), na matokeo yalikuwa ni kumkamata balozi wa Husain Muslim bin Aqiyl na kumnyonga mnamo tarehe 8 ya mwezi wa Dhulhija, yeye pamoja na wakuu wengine, na akalikamata na kulitia jela kundi kubwa la watu na wakuu wa Kufah na hatimaye kutangaza hali ya hatari.